Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA imetoa onyo kwa watumiaji wa simu za mikononi tabia ya kuwasajilia watu wengine laini. Afisa wa maswala ya watumiaji wa bidhaa za mawsiliano kutoka TCRA Bwana Walter Mariki amewataka watumiaji wa simu za mkononi kuacha tabia ya kuwasajilia watu wengine laini za simu ili kuepuka kuhusishwa na makosa ya kimtandao.

Bwana Mariki ametia kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari wa Mkoa wa Katavi na kusema kuwa ni muhimu kwa watumiaji wa simu za mkononi kutoa taarifa sahihi wakati wa usajili.


Aidha kufuatia kuwepo na wimbi la tabia hatarishi katika mitandao mbalimbali ya kijamii naibu mkurugenzi wa TCRA masuala ya watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano Bwana Thadayo Ringo amesisitiza wazazi kufuatilia kwa karibu matumizi ya mitandao kwa watoto.

Post a Comment

Powered by Blogger.