Tweet Share Share Share Share Share Jinsi ya Kuandaa Pilau Unknown January 26, 2018 Pilau ni chakula maalumu kwa waswahili wa pwani ya afrika mashariki ambapo mchele huchanganywa na viungo Mbalimbali na hupikwa kwa mchanganyiko wa nyama, Kuku au Samaki, na pia ni chakula chenye heshima kubwa na ambacho haupaswi kukukosa wakati wa sherehe mbalimbali kubwa. Mahitaji Mchele nusu kilo , Uliosafishwa kwa maji Viazi nusu kilo – menya, na uvisafishe kwa maji Nyama Nusu kilo, Kuku au nyama ya samaki. Kikombe kimoja cha mafuta ya alizeti (au mafuta yeyote ya kula) Vikome 4 vya maji ya moto au Supu Kitunguu 1, kilicho menywa Vijiko 5 vya karafuu iliyosagwa Tangawizi iliyosagwa (kijiko 1 au 2) Nyanya 2, zilizokatwa katika vipande vidogovidogo Viungo vya Pilau Vijiko 2 (Vilivyosagwa) Chumvi na Pilipili kwa ajili ya Kuongeza ladha nzuri Maelekezo Chemsha nyama pamoja na tangawizi kwa dakika 10. Weka Viazi na uache vichemke kwa dakika tano na epua uweke pembeni (tenganusha supu hivyo unaweza kutumia baadaye) Pasha mafuta na weka vitunguu hadi vibadilike rangi na kuwa brown, weka vitunguu na Viungo vya pilau na changanya kwa dakika 1, kwa moto mdogo. Weka nyanya, nyama pamoja na viazi na Koroga Weka mchele na hakikisha mchanganyiko wa kila kitu umechanganyika vizuri kabla ya kuweka supu au maji ya moto, na koroga vizuri. Weka chumvi na pilipili kwa ajili ya Kuongeza ladha, alafu funikia chakula chako kiive kwa moto wa kawaida Chakula chako kikianza kukaukia, Punguzia moto kwa chini, na Funikia Pilau yako, na iache iive kwa dakika 10 Hapo pilau yako itakuwa tayari! Pendezesha Pilau yako kwa kachumbari na Pilipili ya maembe Na ndizi pia inaweza ikatumika ili Kuongeza ladha zaidi Baadhi hupendelea kula Pilau kwa tomato na nyama ya kuku kwa pembeni ambayo nayo ni vizuri zaidi Pilau ni chakula maalumu kwa waswahili wa pwani ya afrika mashariki ambapo mchele huchanganywa na viungo Mbali... Soma zaidi » Mapishi