Tweet Share Share Share Share Share Wenger amtetea Alexis Sanchez baada yake kukosa kupimwa. Unknown January 26, 2018 Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amemtetea mchezaji wa zamani wa klabu hiyo aliyehamia Manchester United baada yake kukosa kipimo muhimu kuhusu matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwilini. Aidha, amesema klabu hiyo haifichi habari zozote kuhusu tukio hilo. Raia huyo wa Chile mwenye miaka 29 anadaiwa kukosa kipimo muhimu Jumatatu siku ambapo alikamilisha uhamisho wake kwenda Manchester United. "Nafikiri lilikuwa tukio la kipekee, kwake kukosa kipimo siku hiyo kwa sababu alikuwa kwingine," amesema Wenger. Mfaransa huyo ameongeza pia kwamba klabu yake haijaombwa ufafanuzi wowote na Chama cha Soka cha England au Shirika la kupambana na matumizi ya dawa zilizoharamishwa michezoni Uingereza. Sanchez alihamia Gunners kutoka Barcelona mwaka 2014, lakini alielekea Old Trafford kwa kubadilishana na mchezaji wa Armenia Henrikh Mkhitaryan. Baada ya taarifa za awali Uhispania, magazeti ya Uingereza Alhamisi yaliripoti kwamba Sanchez alikiuka kanuni FA ya kupatikana wakati wowote ule anapotakiwa kupimwa. Sanchez na Mkhitaryan walipigwa picha wakiwa afisi za uhamiaji Liverpool wakitafuta vibali vya kufanya kazi kabla ya kukamilisha uhamisho wake. Wenger amesema: "Jumatatu kulikuwa na mengi sana yaliyokuwa yanatokea, ni siku ya kipekee sana kwa Alexis Sanchez - kujaza stakabadhi muhimu, vibali vya kazi na usafiri. Alikuwa bado ni mchezaji wetu Jumatatu au la? Huwezi kujua. "Ni siku mbaya tu kwako kutafutwa ukapimwe. Kusema kweli, ukiangalia upande wa usimamizi, huenda ikawa bado ilikuwa ni wajibu wetu kwa kuwa hakuwa amehama. Sijui nini hasa kilitokea. "Sina wasiwasi kwa sababu hatuna chochote cha kuficha, huwa tunajaribu sana kadiri ya uwezo wetu kushirikiana na maafisa wa kupambana na matumizi ya dawa zilizoharamishwa michezoni Uingereza. "Nia ya Alexis haikuwa kujificha na sisi hatuna jambo la kuficha." Sheria zinasemaje? Klabu zinatakiwa kutoa maelezo sahihi ya kina kuhusu vipindi vya mazoezi na walipo wachezaji ili waweze kupimwa wakati wowote ule. Klabu ikikosa kufanya hivyo - au maafisa wa kupima wachezaji washindwe kumpata mchezaji wanayemtafuta - mara tatu kipindi cha miezi 12, basi huchukuliwa kwamba amekiuka sheria za FA. Manchester City na Bournemouth mwaka jana walitozwa faini ya £35,000 kila mmoja na kutahadharishwa baada ya kukiuka kanuni hizo. Arsenal wamemnunua yeyote? Wenger amesema hawapo karibu kumnunua mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang. Ofa yao ya pili ya euro 50m (£43.64m) ilikataliwa wiki hii. Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amemtetea mchezaji wa zamani wa klabu hiyo aliyehamia Manchester United baada yake kukosa kipimo muh... Soma zaidi » Michezo
Tweet Share Share Share Share Share Kocha Arsene Wenger Kafungiwa Mechi Tatu Unknown January 05, 2018 Chama Cha soka cha England FA kimetangaza kumfungia kocha wa club ya Arsenal ya England Arsene Wenger kwa kosa la kutoa maneno yasiokuwa ya kiungwana kwa refa Mike Dean baada ya game ya Arsenal dhidi ya West Ham United iliyomalizika kwa sare ya 1-1.Kocha huyo raia wa Ufaransa alikuwa na hasira dhidi ya refa Mike Dean ambaye aliwapa penati ya utata West Ham United katika mchezo uliyochezwa siku ya mwaka mpya, Wenger amefungiwa kosa pia la kuingia katika chumba cha kubadilishia nguo cha refa Mike Dean.Wenger ambaye amefungiwa mechi tatu na faini ya pound 40,000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 120 baada ya game hiyo alitoa kauli hii ambayo inatafsirika kama kumkosea heshima muamuzi “Maamuzi haya yalikuwa ya kushangaza kidogo, mmemuona (Dean) anafanya anachotaka kitokee, baadhi ya maamuzi msimu huu yamekuwa yakifanywa dhidi yetu sio sawa” Chama Cha soka cha England FA kimetangaza kumfungia kocha wa club ya Arsenal ya England Arsene Wenger kwa kosa la kutoa maneno yasiokuwa ya ... Soma zaidi » Michezo
Tweet Share Share Share Share Share Virgil van Dijk kutua Liverpool kwa pauni Milioni 75 Unknown December 28, 2017 Beki wa kati wa Southampton Virgil van Dijk atajiunga na Liverpool wakati wa dirisha la uhamisho tarehe moja mwezi Januari kwa mkataba wa rekodi ya kimataifa ya £75m. Raia huyo kutoka Uholanzi alitarajiwa kujiunga na Reds msimu uliopita baada ya kuomba uhamisho kutoka kwa klabu yake.Lakini uhamisho huo haukufaulu pale Liverpool ilipoomba msamaha kwa madai ya kumtafuta mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kinyume cha sheria.Ada hiyo ni kubwa ambayo hakuna beki yoyote awewahi kupokea - Manchester City iliipa Monaco £52m kwa Mbeligiji Benjamin Mendy mwezi Julai.Van Dijk amesema kwenye taarifa yake , ''amefurahia'' kusaini kwa mkataba na klabu ya Merseyside na amekiri amekuwa na wakati mgumu '' kwa miezi michache iliyopita'' akiwa Southapton. Beki wa kati wa Southampton Virgil van Dijk atajiunga na Liverpool wakati wa dirisha la uhamisho tarehe moja mwezi Januari kwa mkataba wa re... Soma zaidi » Michezo
Tweet Share Share Share Share Share Carlos Carvalhal kuwa mkufunzi wa Swansea Unknown December 28, 2017 Swansea City wamemteua aliyekuwa mkufunzi wa klabu ya Sheffield Wednesday Carlos Carvalhal kuwa mkufunzi mpya.Kocha mchezaji Leon Britton alikuwa akisimamia Swansea kwa muda tangu klabu hiyo iliopo chini ya jedwali la ligi imfute kazi Paul Clement mnamo tarehe 20 Disemba.Carvalhal, 52, alifutwa kazi na klabu ya Wednesday mkesha wa siku ya krisimasi huku klabu hiyo ya daraja la kwanza ikiwa katika nafasi ya 15 katika jedwali la daraja la kwanza.Raia huyo wa Ureno anajiunga na Swansea hadi mwisho wa msimu akiwa na fursa ya kuongeza mkataba huo.Carvalhal ambaye ni mkufunzi wa tano wa Swansea katika kipindi cha miaka miwili, aliongoza Wednesday kufika katika raundi ya muondoano katika misimu miwili ilopita.Mkufunzi huyo wa zamani wa klabu ya Besikitas , Sporting Lisbon na Maritimo ambaye alirithi mahala pake Stuart Gray huko Hillsborough mwezi Juni 2015 alifanikiwa kupata ushindi wa asilimia 42.7 katika mechi zake 131 alizosimamia. Swansea City wamemteua aliyekuwa mkufunzi wa klabu ya Sheffield Wednesday Carlos Carvalhal kuwa mkufunzi mpya. Kocha mchezaji Leon Britton a... Soma zaidi » Michezo
Tweet Share Share Share Share Share Baada ya Kujifungua Serena Williams Kurudi Uwanjani. Unknown December 25, 2017 Nyota wa tenisi Serena Williams atarejea uwanjani huko Abu Dhabi wiki ijayo miezi minne baada ya kujifungua.Serena mwenye umri wa miaka 36, atakutana mchezaji nambari saba duniani Jelena Ostapenko tarehe 30 Disemba wakati wa mechi ya ubingwa wa dunia ya MubadalaAlijifungua mtoto msichana Alexis Olympia Ohanian mwezi Septemba.Bingwa huyo wa zamani duniani hajacheza tangu alisema Australian Open mwezi Januari.Mkurugenzi wa Australian Open, Craig Tilley amesema kuwa Williama anatarajiwa kutetea taji lake katika mechi ya mwaka 2018 ambayo itaanza Januari 15. Nyota wa tenisi Serena Williams atarejea uwanjani huko Abu Dhabi wiki ijayo miezi minne baada ya kujifungua. Serena mwenye umri wa miaka 36,... Soma zaidi » Michezo
Tweet Share Share Share Share Share Baada ya kupatiwa viwanja na pesa Zanzibar Heroes, Rais Shein amelikubali ombi la kocha wa Zanzibar Heroes. Unknown December 24, 2017 Hii ni baada ya timu ya taifa ya Zanzibar Heroes kumaliza nafasi ya pili katika michuano ya Kombe la CECAFA Senior Challenge Cup 2017, ikifungwa na Kenya katika mchezo wa fainali kwa mikwaju ya penati na kuukosa Ubingwa huo.Timu hiyo iliwasili Zanzibar na kupata mapokezi makubwa licha ya kupoteza mchezo wa fainali kwa penati, ambapo mara nyingi uaminika kuwa inatokea bahati, baada ya mapokezi Rais wa Zanzibar Dr Ally Mohamed Shein ameahidi kutoa viwanja na Tsh milioni 3 kwa msafara wa timu uliyokuwa Kenya.Rais Shein ametoa zawadi ya viwanja na Tsh milioni 3 kwa kila mchezaji na benchi la ufundi jumla watu 33 waliyokuwa sehemu ya timu ya Zanzibar Heroes nchini Kenya.Rais Shein amelikubali ombi la kocha wa Zanzibar Heroes Hemed Morocco la kuomba apewe mualiko Rais wa CAF Ahmad Ahmad ili aje aone vipaji vya Zanzibar ili iwe sehemu ya kumshawishi airudishie Zanzibar uanachama wake wa CAF. Hii ni baada ya timu ya taifa ya Zanzibar Heroes kumaliza nafasi ya pili katika michuano ya Kombe la CECAFA Senior Challenge Cup 2017, ikifu... Soma zaidi » Michezo
Tweet Share Share Share Share Share RATIBA YA MECHI ZOTE ZA KOMBE LA DUNIA, 2018 Unknown December 02, 2017 a a Soma zaidi » Michezo
Tweet Share Share Share Share Share SIMBA WALETA UTATA WA USAJILI WA KIUNGO WAO KWENDA Singida United. Unknown November 29, 2017 HARAKATI za klabu ya Singida United ya Mholanzi Hans Pluijm kumnasa straika wa Simba, Juma Liuzio, ni kama zimegonga mwamba kwa sababu Wekundu hao wa Msimbazi hawataki kumuachia.Singida inamuhitaji Liuzio kwa ajili ya kuongezea nguvu kikosi chake kwenye mzunguko wa pili baada ya kurizishwa na kiwango chake.Rafiki wa karibu wa Liuzio alisema, ni kweli Singida wanamuhitaji mchezaji huyo lakini Simba imeonyesha dalili zote kuwa haitaki kumuachia."Kweli Singida inamtaka, Liuzio lakini Simba wamegoma, hawataki kumtoa sasa sijui kwa nini wakati wenyewe hawampi nafasi kubwa ya kucheza. Bora wangemtoa akajaribu maisha mengine huko,"alisema.Liuzio mchezaji wa zamani wa Mtibwa Sugar, klabu iliyomlea na kumuuza Zesco ya Zambia, alirudi nchini mwaka jana akasajiliwa kwa mkopo na Simba anayoichezea mpaka sasa. HARAKATI za klabu ya Singida United ya Mholanzi Hans Pluijm kumnasa straika wa Simba, Juma Liuzio, ni kama zimegonga mwamba kwa sababu Wekun... Soma zaidi » Michezo
Tweet Share Share Share Share Share “kuondoka kwa Neymar kumetufanya tucheze vizuri,” Messi asema. Unknown November 28, 2017 Mashabiki wengi wa Barcelona walisikitika sana baada ya Neymar kuwaacha na kujiunga na PSG, Neymar alikuwa mchezaji muhimu katika safu ya ushambuliaji ya Barcelona lakini Lioneil Messi ana mawazo tofauti.Lioneil Messi yeye anaona kuondoka kwa Neymar kumewafanya Barcelona wacheze vizuri zaidi haswa eneo lao la ulinzi, Messi anaamini tangu Neymar aondoke safu yao ya ulinzi imekuwa imara zaidi.Tangu Neymar aondoke, kocha wa klabu ya Barcelona Ernesto Valverde amebadili mfumo toka ule uliowafanya MSN kufunga mabao 364 katika miaka mitatu (4-3-3) hadi kuwapeleka katika mfumo mama wa 4-4-2.Lioneil Messi anaamini katika safu yao ya ushambuliaji kuna kitu kimepungua kutokana na kuondoka kwa Neymar lakini timu yao imekuwa na balance nzuri zaidi kati ya ushambuliaji na uzuiaji.Kuhusu timu tishio kwao msimu huu Messi anaamini Man City ni tishio kubwa sana barani Ulaya safari hii na pia PSG, lakini akasisitiza kwamba Real Madrid ni timu kubwa kwahiyo nayo isichukuliwe poa. Mashabiki wengi wa Barcelona walisikitika sana baada ya Neymar kuwaacha na kujiunga na PSG, Neymar alikuwa mchezaji muhimu katika safu ya us... Soma zaidi » Michezo
Tweet Share Share Share Share Share Lwandamina atoa siku 11 za mapumziko Unknown November 27, 2017 KOCHA Mzambia wa Yanga, George Lwandamina ametoa wiki moja ya mapumziko kwa wachezaji wake kufuatia mechi 11 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, timu ikiwa inashika nafasi ya tatu nyuma ya Simba na Azam. Taarifa ya Yanga SC jioni ya leo imesema kwamba kocha Lwandamina ametoa siku saba za mapumziko kwa wachezaji wake kuanzia leo Jumatatu kikosi kitarejea tena mazoezini Jumatatu ijayo.Yanga inakwenda mapumzikoni ikitoka kutoa sare ya kufungana bao 1-1 na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu juzi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.Katika mchezo huo uliochezeshwa na Shomary Lawi wa Kigoma aliyesaidiwa na Abdallah Rashid wa Pwani na Sylvester Mwanga wa Kilimanjaro, Prisons walitangulia kwa bao la Eliuter Mpepo dakika ya tisa akitumia makosa ya mabeki wa kati wa Yanga, Andrew Vincent ‘Dante’ na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ waliochanganyana na kipa wao, Mcameroon, Youth Rostande na kushindwa kuokoa.Prisons walipata pigo dakika ya 36 baada ya mchezaji wake, Lambert Sibiyanka kutolewa kwa kadinyekundu na refa Lawi kufuatia kumpiga kiwiko beki wa Yanga, Juma Abdul.Yanga walitumia mwanya huo kuongeza mashambulizi kusaka bao la kusawazisha na wakafanikiwa kupata bao dakika ya 41, lililofungwa na kiungo Raphael Daudi aliyemalizia krosi ya mshambuliaji Ibrahim Ajib.Kwa sare hiyo, Yanga inafikisha pointi 21 baada ya kucheza mechi 11, ikizidiwa pointi mbili mbili na Simba na na moja na Azam. KOCHA Mzambia wa Yanga, George Lwandamina ametoa wiki moja ya mapumziko kwa wachezaji wake kufuatia mechi 11 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania... Soma zaidi » Michezo
Tweet Share Share Share Share Share Taji la Miss Universe 2017, latua kwa Mrembo wa Afrika Kusini. Unknown November 27, 2017 Ni furaha kubwa kusikia nchi yenu imefanikiwa kuzibwaga nchi nyingine katika mashindano ya dunia. Shangwe limetawala nchini Afrika Kusini baada ya mrembo wao Demi-Leigh Nel-Peters kufanikiwa kushinda taji la Miss Universe kwa mwaka huu.Demi ambaye ana umri wa miaka 22, amefanikiwa kutwaa taji hilo Jumapili hii mjini Las Vegas nchini Marekani ambapo shindano hilo lilipokuwa linafanyika.Mrembo huyo alifanikiwa kuwabwaga washiriki wengine ambao waliingia katika hatua ya tano bora akiwemo mrembo kutoka Colombia, Jamaica, Thailand na Venezuela.Washiriki wa Miss Universe ambao walifanikiwa kuingia kwenye tano bora. Ni furaha kubwa kusikia nchi yenu imefanikiwa kuzibwaga nchi nyingine katika mashindano ya dunia. Shangwe limetawala nchini Afrika Kusini ba... Soma zaidi » Michezo
Tweet Share Share Share Share Share southampton yaipa kichapo Everton. Unknown November 26, 2017 Matatizo ya Everton chini ya Meneja David Unsworth yameendelea kudhihirika kwenye English Premium League (EPL) baada ya hapo jana kupokea kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwa Southampton katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la St Marys.Goli la uongozi liliwekwa kimiani na Dusan Tadic na Mshambuliaji wa Saints, Charlie Austin amefunga magoli mawili kwa kichwa katika ki yapindi cha pili ya mechi hiyo, na hapo baadae Steven Davis kuhitimisha karamu ya magoli baada kukamilisha hesabu ya bao la 4 dakika ya 87.Mchezaji wa Everton aliyelipiwa gharama ya juu kuliko mchezaji mwingine katika klabu hiyo Gylfi Sigurdsson alisawazisha mambo kabla ya kipenga cha mapumziko lakini Southampton wakafyetuka kwa kasi baada ya mapumziko hayo.Bao la kusawazisha kwa Everton lilifungwa na mchezaji Gylfi Sigurdsson mda mchache kabla ya kipenga cha mwamuzi kuelekea Mapumziko Matatizo ya Everton chini ya Meneja David Unsworth yameendelea kudhihirika kwenye English Premium League (EPL) baada ya hapo jana kupokea ki... Soma zaidi » Michezo
Tweet Share Share Share Share Share Mshambuliaji kutoka Ghana rasmi Azam FC Unknown November 26, 2017 Mghana Bernard Arthur, mshambuliaji mpya wa Azam FC amewasili asubuhi ya leo Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam tayari kuanza maisha mapya na Azam FC ndani ya Chamazi.Arther aliyesaini miaka miwili na klabu ya Azam FC akitokea kwenye timu ya Liberty Professional ya kwao, Ghana, amewasili leo akiongozana na Mtendaji Mkuu wa Azam, Abdul Mohamed ambaye alimfuata nchini humo kukamilisha usajili wake.Akizumgumza jijini Dar es Salaam leo, Ofisa Habari wa Azam, Jafari Idd alisema kuwa, mchezaji huyo raia wa Ghana tayari ameungana na timu huku akisubiri uongozi wa klabu hiyo wakishughulikia vibali yake kwa ajili ya kuanza kazi rasmi na matajiri hao wa chamazi.“Mchezaji wetu mpya wa Ghana, amewasili alfajiri ya leo nchini akiwa na Mtendaji mkuu wa Azam, Abdul Mohamed, tayari ameungana na timu Chamazi huku akisubiri uongozi kushughulikia vibali vyake ili aweze kuanza kazi rasmi,” alisema Jafari.Usajili wa Arthur ni sehemu ya mapendekezo ya benchi la ufundi la timu hiyo kwenye usajili huu wa dirisha dogo, anayekuja kuziba pengo la straika mwingine, Yahaya Mohammed, aliyeondoka kwa makubaliano maalumu ya pande mbili wiki chache zilizopita.Mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya WAFA (Ghana) na Asec Mimosa ya Ivory Coast, anaungana na washambuliaji wengine wa timu hiyo katika kukiongezea makali kikosi hicho, ambao ni Mbaraka Yusuph, Wazir Junior, Yahya Zayd, Shaaban Idd pamoja na wale waliopandishwa kutoka Azam B, Paul Peter na Andrea Simchimba.Hadi sasa timu inajiandaa kwa ajili ya mechi yao ya kesho dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro, katika mchezo wa raundi ya 11 ya Ligi Kuu Bara utakaopigwa kuanzia majira saa moja usiku kwenye Uwanja wao wa nyumbani Azam Complex uliopo Chamazi.Wakati huo, nyota wawili wa Azam FC, Shaaban Idd na Joseph Kimwaga, ambao ni majeruhi sasa huenda wakarejea dimbani Januari Mosi mwakani wakati timu hiyo itakapokuwa ikishiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar. Mghana Bernard Arthur, mshambuliaji mpya wa Azam FC amewasili asubuhi ya leo Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam t... Soma zaidi » Michezo
Tweet Share Share Share Share Share CAF yataka Yanga, Simba Kupeleka Majina Unknown November 25, 2017 Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limezitaka Simba na Yanga haraka kupeleka majina ya wachezaji wake kwa Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kwa ajili ya ushiriki wa michuano yake mwakani, pia watakaguliwa mahesabu yao.Yanga itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuwa bingwa wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, huku Simba wakishiriki Kombe la Shirikisho kutokana na kuwa mabingwa wa Kombe la FA.Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, alisema klabu hizo zinatakiwa kuwasilisha majina yao Caf mapema kabla ya mwisho wa mwezi huu.“Simba na Yanga wanatakiwa kutuma majina ya usajili wa wachezaji wao mapema kabla ya Novemba 30, mwaka huu kwa sababu wakichelewa inawezakuwa tatizo kwao,” alisema Lucas. “Na kwa sasa kamati ya leseni za klabu inakwenda kufanya ukaguzi katika klabu hizo ili kufahamu kama zimetimiza matakwa ya kupata leseni ya kushiriki michuano ya Caf.“Timu zitakaguliwa ofisini na watendaji wake, umiliki wa nyaraka mbalimbali, ukaguzi wa mahesabu na ripoti ya fedha ya mwaka mzima kama Kanuni ya 11 ya ligi kuu na kanuni ya saba ya Caf zinavyojieleza kuhusiana na leseni za klabu,” alisema Lucas. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limezitaka Simba na Yanga haraka kupeleka majina ya wachezaji wake kwa Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kwa... Soma zaidi » Michezo
Tweet Share Share Share Share Share Kocha K'Njaro Stars kuwapeleka wachezaji Ulaya Unknown November 24, 2017 Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania bara Kilimanjaro Stars Ammy Ninje, amesema yupo tayari kuwasaidia wachezaji wa Tanzania kwenda kucheza soka barani Ulaya.Ammy Ninje ambaye ataiongoza timu hiyo kwenye michuano ya CECAFA Challenge nchini Kenya mapema mwezi ujao amesema yeye yupo tayari kutumia uzoefu wake barani Ulaya kuwatafutia timu wachezaji watakaoonesha viwango.“Mimi nina ‘Network’ ya walimu wenzangu kwenye nchi za Ulaya kama Sweden, hivyo nitawasaidia wachezaji wenye vipaji vya kucheza Ulaya kuweza kupata vilabu ili wakacheze soka la kulipwa, na kama nchi tuwe na ‘professional’ wengi”, amesema Ammy Ninje.Kocha huyo ameyasema hayo kwenye mahojiano na kipindi cha Hotmix jioni ya leo Novemba 24, ambapo amesema yupo tayari kutumia uzoefu wake wote ili nchi ifanikiwe na kufikia viwango vya mataifa kama Uganda na zaidi ya hapo.Kuhusu michuano ya Challenge Ninje, amesema atajipanga vyema na kikosi cha wachezaji 20 ambao aliwataja hivi karibuni kwaajili ya michuano hiyo na anaamini wakishirikiana vyema wataibuka mabingwa.Michuano hiyo inatarajiwa kuanza Desemba 3 na kumalizika Desemba 17 nchini Kenya ambapo Tanzania ipo kundi moja na timu za Zanzibar Heroes, Rwanda, Libya na wenyeji Kenya. Kilimanjaro Stars itacheza mchezo wa ufunguzi Desemba 3 dhidi ya Libya. Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania bara Kilimanjaro Stars Ammy Ninje, amesema yupo tayari kuwasaidia wachezaji wa Tanzania kwenda kuche... Soma zaidi » Michezo
Tweet Share Share Share Share Share Beki wazamani wa Simba afanyiwa Upasuaji Ujerumani. Unknown November 24, 2017 Beki wa zamani wa Simba, Emily Mugeta ambaye sasa anakipiga katika timu ya daraja la tano nchini Ujerumani, amefanyiwa upasuaji wa bega. Mugeta ambaye aliwahi kucheza Simba akianzia timu ya vijana, amefanyiwa upasuaji huo leo. “Bega lilinisumbua sana hata kabla sijaja timu hii, lakini mwisho nimepata matibabu na mwisho ni huu upasuaji. Nashukuru kila kitu kimeenda vizuri,” alisema Mugeta. Beki wa zamani wa Simba, Emily Mugeta ambaye sasa anakipiga katika timu ya daraja la tano nchini Ujerumani, amefanyiwa upasuaji wa bega. Mu... Soma zaidi » Michezo