Pilau ni chakula
maalumu kwa waswahili wa pwani ya afrika mashariki ambapo mchele huchanganywa
na viungo Mbalimbali na hupikwa kwa
mchanganyiko wa nyama, Kuku au Samaki, na pia ni chakula chenye heshima kubwa
na ambacho haupaswi kukukosa wakati wa sherehe mbalimbali kubwa.
Mahitaji
- Mchele nusu kilo , Uliosafishwa kwa maji Viazi nusu kilo – menya, na uvisafishe kwa maji Nyama Nusu kilo, Kuku au nyama ya samaki. Kikombe kimoja cha mafuta ya alizeti (au mafuta yeyote ya kula) Vikome 4 vya maji ya moto au Supu Kitunguu 1, kilicho menywa Vijiko 5 vya karafuu iliyosagwa Tangawizi iliyosagwa (kijiko 1 au 2) Nyanya 2, zilizokatwa katika vipande vidogovidogo Viungo vya Pilau Vijiko 2 (Vilivyosagwa) Chumvi na Pilipili kwa ajili ya Kuongeza ladha nzuri
Maelekezo
Chemsha nyama pamoja na
tangawizi kwa dakika 10. Weka Viazi na uache vichemke kwa dakika tano na epua uweke pembeni (tenganusha supu hivyo
unaweza kutumia baadaye)
Pasha mafuta na weka vitunguu hadi vibadilike rangi na
kuwa brown, weka vitunguu na Viungo vya pilau na changanya kwa dakika 1, kwa
moto mdogo.
Weka nyanya, nyama
pamoja na viazi na Koroga
Weka mchele na
hakikisha mchanganyiko wa kila kitu umechanganyika vizuri kabla ya kuweka supu
au maji ya moto, na koroga vizuri.
Weka chumvi na pilipili
kwa ajili ya Kuongeza ladha, alafu funikia chakula chako kiive kwa moto wa
kawaida
Chakula chako kikianza
kukaukia, Punguzia moto kwa chini, na Funikia Pilau yako, na iache iive kwa dakika
10
Hapo pilau yako itakuwa
tayari!
Pendezesha Pilau yako
kwa kachumbari na Pilipili ya maembe
Na ndizi pia inaweza
ikatumika ili Kuongeza ladha zaidi
Baadhi hupendelea kula Pilau kwa tomato na
nyama ya kuku kwa pembeni ambayo nayo ni vizuri zaidi
Post a Comment