Meneja
wa Arsenal Arsene Wenger amemtetea mchezaji wa zamani wa klabu hiyo aliyehamia
Manchester United baada yake kukosa kipimo muhimu kuhusu matumizi ya dawa za
kuongeza nguvu mwilini.
Aidha, amesema klabu hiyo haifichi habari zozote
kuhusu tukio hilo.
Raia huyo wa Chile mwenye miaka 29 anadaiwa kukosa
kipimo muhimu Jumatatu siku ambapo alikamilisha uhamisho wake kwenda Manchester
United.
"Nafikiri lilikuwa tukio la kipekee, kwake kukosa
kipimo siku hiyo kwa sababu alikuwa kwingine," amesema Wenger.
Mfaransa huyo ameongeza pia kwamba klabu yake
haijaombwa ufafanuzi wowote na Chama cha Soka cha England au Shirika la
kupambana na matumizi ya dawa zilizoharamishwa michezoni Uingereza.
Sanchez alihamia Gunners kutoka Barcelona mwaka
2014, lakini alielekea Old Trafford kwa kubadilishana na mchezaji wa Armenia
Henrikh Mkhitaryan.
Baada ya taarifa za awali Uhispania, magazeti ya
Uingereza Alhamisi yaliripoti kwamba Sanchez alikiuka kanuni FA ya kupatikana
wakati wowote ule anapotakiwa kupimwa.
Sanchez na Mkhitaryan walipigwa picha wakiwa afisi
za uhamiaji Liverpool wakitafuta vibali vya kufanya kazi kabla ya kukamilisha
uhamisho wake.
Wenger amesema: "Jumatatu kulikuwa na mengi
sana yaliyokuwa yanatokea, ni siku ya kipekee sana kwa Alexis Sanchez - kujaza
stakabadhi muhimu, vibali vya kazi na usafiri. Alikuwa bado ni mchezaji wetu
Jumatatu au la? Huwezi kujua.
"Ni siku mbaya tu kwako kutafutwa ukapimwe.
Kusema kweli, ukiangalia upande wa usimamizi, huenda ikawa bado ilikuwa ni
wajibu wetu kwa kuwa hakuwa amehama. Sijui nini hasa kilitokea.
"Sina wasiwasi kwa sababu hatuna chochote cha
kuficha, huwa tunajaribu sana kadiri ya uwezo wetu kushirikiana na maafisa wa
kupambana na matumizi ya dawa zilizoharamishwa michezoni Uingereza.
"Nia ya Alexis haikuwa kujificha na sisi hatuna
jambo la kuficha."
Sheria zinasemaje?
Klabu zinatakiwa kutoa maelezo sahihi ya kina kuhusu
vipindi vya mazoezi na walipo wachezaji ili waweze kupimwa wakati wowote ule.
Klabu ikikosa kufanya hivyo - au maafisa wa kupima
wachezaji washindwe kumpata mchezaji wanayemtafuta - mara tatu kipindi cha
miezi 12, basi huchukuliwa kwamba amekiuka sheria za FA.
Manchester City na Bournemouth mwaka jana walitozwa
faini ya £35,000 kila mmoja na kutahadharishwa baada ya kukiuka kanuni hizo.
Arsenal wamemnunua yeyote?
Wenger amesema hawapo karibu kumnunua mshambuliaji
wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang. Ofa yao ya pili ya euro 50m
(£43.64m) ilikataliwa wiki hii.
Post a Comment