Matatizo ya Everton chini ya Meneja David Unsworth yameendelea kudhihirika kwenye English Premium League (EPL) baada ya hapo jana kupokea kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwa Southampton katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la St Marys.

Goli la uongozi liliwekwa kimiani na Dusan Tadic na Mshambuliaji wa Saints, Charlie Austin amefunga magoli mawili kwa kichwa katika ki yapindi cha pili ya mechi hiyo, na hapo baadae Steven Davis kuhitimisha karamu ya magoli baada kukamilisha hesabu ya bao la 4 dakika ya 87.

Mchezaji wa Everton aliyelipiwa gharama ya juu kuliko mchezaji mwingine katika klabu hiyo Gylfi Sigurdsson alisawazisha mambo kabla ya kipenga cha mapumziko lakini Southampton wakafyetuka kwa kasi baada ya mapumziko hayo.

Bao la kusawazisha kwa Everton lilifungwa na mchezaji Gylfi Sigurdsson mda mchache kabla ya kipenga cha mwamuzi kuelekea Mapumziko


Post a Comment

Powered by Blogger.