Hii ni baada ya kutangaza kujivua uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) siku ya Jumatano Davidi Kafulila na leo kukabidhiwa kadi ya uanachama ndani ya CCM.

Kafulila alikabidhiwa kadi ya uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Katibu Mwenezi wa CCM, ndg Humphrey Polepole katika mkutano wa kumnadi mgombea wa udiwani wa chama hicho, kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani katika Kata ya Mbweni jijini Dar es salaam.


Hapo awali Kafulila aliwahi kuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kisha kufukuzwa na baadae kujiunga na Chama cha NCCR Mageuzi ambapo alifanikiwa kuwa Mbunge wa Kigoma Kusini mwaka 2010-2015 kwa tiketi ya chama cha NCCR Mageuzi na baadaye kurudi tena Chadema 2016 na hapo juzi jumatano alitangaza kukihama chama hicho kwa madai  ya kuwa upinzani hauna nia ya kupambana na ufisadi.


Kwa upande wa mkewe ambaye ni Mbunge Viti Maalumu kupitia chama cha CHADEMA, Jesca Kishoa juzi wakati akizungumza na wanahabari alipingana na kauli ya mumewe na kusema kwamba, mumewe anapaswa kusema ukweli na kwamba sababu alizozisema sizo zilizomuondoa ndani ya chama hicho huku akiongeza kwamba mume wake hana msimamo.



Kafulila amekabidhiwa kadi hiyo ya CCM ikiwa imebaki siku moja kabla ya kuhitimishwa kwa kampeni za uchaguzi mdogo wa marudio ya nafasi za udiwani kwa Kata 43 ndani ya Tanzania.

Post a Comment

Powered by Blogger.