Hii ni baada ya wanasayansi kusema kwamba ziwa kubwa zaidi barani Afrika ziwa Victoria linalounganisha nchi za Tanzania, Kenya na Uganda, lipo katika hatari kubwa ya kukauka kwa maji yake.

Wanasema kwamba sababu kubwa. itakayopelekea ziwa kukauka ni uvuvi haramu na uliopitiliza pamoja na uvamizi wa mazingira kuzunguka maeneo ya ziwa.
Maji machafu pia yanayotiririshwa kuelekea kwenye ziwa yanahatarisha usalama wa viumbe wanaopatikana katika ziwa hilo.

Kwa upande wa pili jeshi la Uganda limeweka mipango maalum ikiwa ni pamoja na kuharibu nyenzo za uvuvi zinazotajwa kuwa miongoni mwa sababu.
 

Post a Comment

Powered by Blogger.