Tweet Share Share Share Share Share Kenyatta ateua mawaziri wapya Kenya, na balozi mpya Tanzania. Unknown January 26, 2018 Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza watu anaopendekeza waidhinishwe kuwa mawaziri katika serikali yake mpya baada yake kushinda uchaguzi mwaka jana. Mawaziri sita ambao walikuwa wanahudumu katika serikali yake muhula uliopita wamevuliwa uwaziri na kuteuliwa kuwa mabalozi. Bw Dan Kazungu, ambaye amekuwa waziri wa madini, amependekezwa kuwa balozi mpya wa Kenya nchini Tanzania. Aliyekuwa balozi wa Kenya nchini humo Chirau Ali Mwakwere alijiuzulu mwaka jana ili kuwania kiti cha ugavana katika uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti. Alishindwa kwenye uchaguzi huo. Miongoni mwa walioteuliwa kuwa mawaziri wapya ni mwanahabari mkongwe Farida Karoney ambaye ameteuliwa kuwa waziri wa ardhi. Wadhifa huo ulikuwa unashikiliwa na Prof Jacob Kaimenyi ambaye amependekezwa kuwa balozi wa Kenya katika Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Sayansi, Elimu na Utamaduni (Unesco) mjini Geneva. Bi Monica Juma ameteuliwa kuwa waziri mpya wa mambo ya nje kuchukua nafasi ya Amina Mohamed ambaye amependekezwa kuwa waziri wa elimu. Mawaziri walioteuliwa kuwa mabalozi Judi Wakhungu (Mazingira) - Ufaransa Cleopa Mailu (Afya) - Umoja wa Mataifa mjini Geneva Dan Kazungu (Madini) - Tanzania Phylis Kandie (Leba na Jumuiya ya Afrika Mashariki) - Ubelgiji, Luxemburg na Umoja wa Ulaya Willy Bett (Kilimo) - India Jacob Kaimenyi (Ardhi) -UNESCO, Paris Hassan Wario (Michezo) - Austria Kwa sasa, orodha kamili ya mawaziri waliopendekezwa ni: Adan Mohammed - Viwanda Amina Mohammed - Elimu Charles Keter - Kawi Eugene Wamalwa - Ugatuzi Farida Karoney - Ardhi Fred Matiangi - Masuala ya Ndani na Usalama Henry Rotich - Fedha (Hazina Kuu) James Macharia - Uchukuzi John Munyes - Madini na Mafuta Joseph Mucheru - Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Keriako Tobiko - Mazingira Margaret Kobia - Vijana na Utumishi wa Umma Monica Juma -Mambo ya Nje Mwangi Kiunjuri - Kilimo Najib Balala - Utalii Peter Munya - Jumuiya ya Afrika Mashariki Racheal Omamo - Ulinzi Raphel Tuju - Waziri (Bila wizara kwa sasa) Rashid Achesa - Michezo Sicily Kariuki - Afya Simon Chergui - Maji Ukur Yattany - Leba Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza watu anaopendekeza waidhinishwe kuwa mawaziri katika serikali yake mpya baada yake kushinda ... Soma zaidi » Kimataifa
Tweet Share Share Share Share Share Papa Francis Ametoa Mwito wa Kuwepo Amani Katika Mji wa Jerusalem Unknown December 25, 2017 Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis jana ametoa mwito wa kuwepo amani katika mji wa Jerusalem wakati wa salamu zake za Krismasi.Na kuelezea hali watoto wanayokabiliwa nayo katika maeneo yenye migogoro huku pia akitoa mwito kwa waumini bilioni 1.3 wa kanisa katoliki duniani kote kutowapuuza wahamiaji. Akiwahutubia mamia kwa maelfu ya waumini wa kanisa hilo mjini Vatican Papa Francis ametoa mwito wa amani mjini Jerusalem na katika ardhi yote takatifu. Amesema ulimwengu unashuhudia watoto katika Mashariki ya Kati wakiendelea kuteseka kwasababu ya mivutano kuongezeka kati ya waisrael na wapalestina. Papa Francis amesema ulimwengu unapaswa kuomba ili majadiliano ya pande zinazovutana yarejee na hatimaye suluhisho la mataifa mawili lipatikane na ambalo litatambuliwa kimataifa.Ujumbe huo wa papa katika mkesha wa krismasi umekuja mnamo wakati mivutano mipya ikiibuka katika ukingo wa magharibi kufuatia rais Donald Trump kutangaza kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel huku pia rais wa Guatemala Jimmy Morales akisema nchi yake itahamishia ubalozi wake mjini humo. Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis jana ametoa mwito wa kuwepo amani katika mji wa Jerusalem wakati wa salamu zake za Kri... Soma zaidi » Kimataifa
Tweet Share Share Share Share Share Uingereza Yaizuia Manowari ya Urusi North Sea Unknown December 25, 2017 Monowari ya jeshi la wa wanamaji wa Uingereza iliisindikiza ile ya Urusi katika bahari ya North Sea karibu na maji ya Uingereza siku ya Krismasi, kwa mujibu wa jeshi la wanamaji wa Uingrreza. Ilisema kuwa HMS St Albans ilisindikiza Admiral Gorshkov katika sehemu zilizo karibu na maji yake.Urusi haijatamka lolote kuhusu kuhusu suala hilo.Jeshi la Uingereza lilisema kuwa kumekwa na visa hivi karibuni ambapo vyombo vya majini vya Urusi vinapita karibu na maji ya Uingereza.Mkuu wa jeshi la ulinzia nchini Uingereza Sir Stuart Peach, mapema mwezi huu alisema kuwa Uingereza na Nato wanahitaji kuweka kipaumbele suala la kulinda nyaya za mawasiliano ya mtandao zinazopiti baharini. Alisema kuwa itakuwa piga kubwa na baya kwa uchumi ikiwa nyaya hizo zinatakatwa au kuharibiwa.Nyanya hizo uunganisha sehemu tofauti za dunia kati ya nchi na mabara.Katika taarifa jeshi la majini la Uingereza lilisema kwa HMS St Albans iliitwa tarehe 23 Disemba, kupiga doria na kuifuata manowari mpya ya Urusi ya Admiral Gorshkov ikipitia bahari karibu na maji ya Uingereza.Lilisema kuwa meli hiyo ilisalia baharini siku ya Krismasi, ikichunguza chombo hicho cha Urusi."Sitakawia kulinda maji au kuvumilia uchokozi wowote," waziri wa ulinzi Gavin Williamson alisema. Monowari ya jeshi la wa wanamaji wa Uingereza iliisindikiza ile ya Urusi katika bahari ya North Sea karibu na maji ya Uingereza siku ya Kris... Soma zaidi » Kimataifa
Tweet Share Share Share Share Share Ubalozi wa Guatemala Kuhamishiwa Jerusalem Unknown December 25, 2017 Rais wa Guatemala Jimmy Morales ameamrisha ubalozi wa nchi hiyo nchini Israel kuhamishwa kwenda Jurusalen.Katika ujumbe kupitia Facebook, Bw. Morales alisema kuwa hatua hiyo ilichukuliwa baada ya kuzungumza na waziri mkuu Benjamin Netanyahu.Wiki iliyopita Guatemala ilikuwa moja ya nchi tisa zilizopiga kura kupinga azimio la Umoja wa Mataifa la kuitaka Marekani kufuta hatua ya kuitambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.Donald Trump alitishia kupunguza misaada kwa nchi ambazo zilipiga kura dhidi ya Marekani.Marekani ni mtoaji muhimu wa misaada kwa Guatemala, nchi maskini ya kati kati mwa Amerika.Siku ya Jumapili Bw. Morales alisema kuwa alikuwa ameamrisha mmlaka za nchi hiyo kufanya mikakati ya kuhamisha ubalozi kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem.ali ya mji wa Jerusalem ndio chanzo cha mzozo kati ya Israel na Palestiona.Israel ilitwaa mji huo ambao awali ulikuwa ukikaliwa na Jordan wakati wa vita vya mwaka 1967 vya Mashariki ya Kati na inaitaja mji wote huo kuwa mji wake mkuu.Wapalestina wanadai kuwa East Jerusalem ni mji wao mkuu taifa lake la baadaye.Jerusalem haujatambuliwa kimataifa na nchi zote kwa sasa zina balozi zao huko Tel Aviv. Rais wa Guatemala Jimmy Morales ameamrisha ubalozi wa nchi hiyo nchini Israel kuhamishwa kwenda Jurusalen. Katika ujumbe kupitia Facebook , ... Soma zaidi » Kimataifa
Tweet Share Share Share Share Share Liberia kupiga kura katika uchaguzi wa urais Jumatano tarehe 27/12/2017. Unknown December 24, 2017 Waliberia watamchagua kiongozi mpya Jumatano ya tarehe 27/12/2017 katika uchaguzi wa duru ya pili kati ya makamu wa rais Joseph Boakai na mchezaji kandanda wa zamani maarufu George Weah.Kura hiyo itaashiria mabadiliko ya kwanza ya uongozi nchini humo tangu mwaka 1944.Baada ya wiki saba za uchelewesho kutokana na malalamiko ya kisheria yaliyofikishwa mahakamani na chama tawala cha Boakai cha Unity dhidi ya tume ya uchaguzi nchini humo, vituo vya kupigia kura vinatarajiwa kufunguliwa kuanzia saa mbili asubuhi saa za Liberia na kufungwa majira ya saa 12 jioni kwa ajili ya wapigakura milioni 2.1 waliandikishwa kupiga kura.Chama cha Weah cha Muungano kwa ajili ya mabadiliko ya kidemokrasi, Coalition for Democratic Change (CDC) kimewataka wapiga kura kutokunywa pombe kupita kiasi katika sikukuu ya Krismasi na kuamka mapema siku ya tarehe 26 kupiga kura zao katika kile mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya taifa NEC, Francis Korkoya alichosema kuwa ni "kujitolea mhanga kwa ajili ya demokrasia yetu na nchi yetu."Watachagua mrithi wa rais Ellen Johnson Sirleaf, anayetarajiwa kuondoka madarakani mwezi Januari baada ya miaka 12 akiwa katika uongozi wa juu wa taifa hilo la Afrika Magharibi, linaloibuka kutoka katika mavumbi ya vita vya wenyewe kwa wenyewe,(1989-2003) na pia kushughulikia hatua za kupambana na mzozo wa ugonjwa wa Ebola (2014-16). Waliberia watamchagua kiongozi mpya Jumatano ya tarehe 27/12/2017 katika uchaguzi wa duru ya pili kati ya makamu wa rais Joseph Boakai na m... Soma zaidi » Kimataifa
Tweet Share Share Share Share Share Korea Kaskazini wamesema Vikwazo vipya vya UN ni kama vita. Unknown December 24, 2017 Baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa lilitangaza vikwazo vipya siku ya Ijumaa kufuatia majaribio ya makombora ya masafa marefu ya Korea Kaskazini.Korea Kaskazini imetaja vikwazo vya hivi majuzi vya Umoja wa Mataifa dhidi yake ni kama vita.Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ilisema kuwa hatua hizo zilikuwa ni kubwa na ngumu kwa uchumi kwa mujibu wa shirika la KNCA la Korea Kaskazini.Iliongeza kuwa kuwa kuongeza msimamo mkali zaidi wa Korea Kaskazini ndilo jibu kwa Marekani.Marekani ilipendekeza vikwazo hivyo na kuungwa mkono na wanacha wote 15 wa baraza la usalama la Umoja Mataifa vikiwemo vya kukata mauzo ya mafuta kwa asilimia 90 kwa Korea Kaskazini.Korea Kaskazini tayari iko chini ya vikwami kutoka Marekani, Umoja wa Mataifa na EU. Baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa lilitangaza vikwazo vipya siku ya Ijumaa kufuatia majaribio ya makombora ya masafa marefu ya Korea Kask... Soma zaidi » Kimataifa
Tweet Share Share Share Share Share Jeshi la Argentina lasitisha zoezi la kutafuta manowari iliyopotea. Unknown November 30, 2017 Jeshi la wana maji la Argentina limesitisha jitihada za kutafuta Monowari iliyopotea kusini mwa bahari ya Atlantiki wiki mbili zilizopita ikiwa na watu 44.Msemaji wa kikosi cha jeshi la wana maji, Keptein Enrique Balbi amesema kwa sasa shughuli hiyo imeitishwa rasmi.Kaptain Enrique Balbi, anasema kuwa kikosi cha uokoaji chenye idadi ya watu 4000 kilikwenda kufanya uokoaji mara mbili.Balbi anasema kuwa pamoja na jitihada za uokoaji zilizofanyika lakini,hakujawa na mafanikio ya kufanikiwa.Hata hivyo matumaini ya kuwapa waliokuwa nadani ya nyambizi hiyo wakiwa hai, yalitoweka baada ya kudaiwa kusikika mlipuko mkubwa karibu na eneo ambalo ilikuwa inasadikika kwamba ndipo ilipo manuari hiyo iliyozama.Nyambizi hiyo ya ARA San Juan ilikumbwa na mkasa huo ilipokuwa ikirejea kutoka katika shughuli zake za kawaida keneo la Ushuaia. Jeshi la wana maji la Argentina limesitisha jitihada za kutafuta Monowari iliyopotea kusini mwa bahari ya Atlantiki wiki mbili zilizopita ik... Soma zaidi » Kimataifa
Tweet Share Share Share Share Share Wakuu wa jeshi wateuliwa kuwa mawaziri Zimbabwe. Unknown November 30, 2017 Rais mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amelitaja baraza lake la mawaziri akimteua afisa mkuu wa jeshi kwa wadhfu mkuu katika serikali yake.Waziri mpya wa fedha ni Sibusiso Moyo , jenerali aliyetangaza katika runinga ya taifa hilo wiki mbili zilizopita kwamba jeshi limechukua udhibiti.Mkuu wa jeshi la angani Perence Shiri ataongoza wizara ya fedha na kilimo.Kiongozi mmoja wa upinzani Tendai Biti amesema kuwa fungate iliokuwa ikisherehekewa Zimbabwe imeisha kabla ya kuanza.Zimbabwe: '' mamba'' huenda akaiongoza ZimbabweWapinzani waandamana ZimbabweWasioiheshimu bendera Zimbabwe kuadhibiwaBwana Mnangagwa aliapishwa wiki moja iliopita kufuatia kujiuzulu kwa Robert Mugabe ambaye alikuwa mamlakani kwa takriban miaka saba. Rais mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amelitaja baraza lake la mawaziri akimteua afisa mkuu wa jeshi kwa wadhfu mkuu katika serikali yake... Soma zaidi » Kimataifa
Tweet Share Share Share Share Share Marekani yaitaka dunia kusitisha biashara na Korea Kaskazini. Unknown November 30, 2017 Marekani imetoa wito kwa mataifa mbalimbai kukata uhusiano wake wa kidiplomasia na kibiashara na Korea Kaskazini, ikiwa ni hatua ya kupinga majaribio ya makombora ambayo yamekuwa yakifanywa na taifa hilo.Balozi wa Marekani Nikki Haley, ametoa pendekezo hilo katika mkutano wa dharura wa baraza la usalama la umoja wa mataifa unaoendelea mjini New York.Bi. Haley amesema kuwa Rais wa Marekani amemtaka Rais wa China Xi Jinping kusitisha biashara ya mafuta ghafi na Korea Kaskazini, kama sehemu ya kutekeleza hatua ya kuwekewa vikwazo kwa taifa hilo.Kupitia hatua hii ya kuiwekea vikwazo Korea Kaskazini tunapaswa kusitisha asilimia tisini ya biashara na Korea Kaskazini pamoja na asilimia 30 yamafuta yake.Mwaka 2003, China ilisitisha kupelekea mafuta Korea Kaskazini ,muda mfupi baadaye taifa hilo likasogea katika meza ya majadiliano.''Tumefikia hatua ya kuitaka China kuchukua hatua Zaidi katika hili, ni lazima isitishe kuipatia mafuta Korea Kaskazini," alisema Haley.Wajumbe wa baraza la usalama la umoja wa mataifa wanakutana mjini Ne York kujadili hatua ya Korea kaskazini na majaribio ya makombora ya masafa marefu.Msemaji wa katibu mkuu wa umoja wa Stéphane Dujarric, amesema kuwa Antonio Guterres, amelaani hatua hiyo Korea Kaskazini na kuongeza kuwa huo ni ukiukaji wa maamuzi ya baraza la usalama la umoja wa mataifa. Marekani imetoa wito kwa mataifa mbalimbai kukata uhusiano wake wa kidiplomasia na kibiashara na Korea Kaskazini, ikiwa ni hatua ya kupinga ... Soma zaidi » Kimataifa
Tweet Share Share Share Share Share Apoteza Maisha baada ya kunywa sumu mahakamani. Unknown November 29, 2017 Kikao cha kusikiliza rufaa iliyowasilishwa na washtakiwa wa uhalifu wa kivita mjini The Hague, Uholanzi kimesitishwa ghafla baada ya mmoja wa washtakiwa kusema amekunywa sumu baada ya kusikiliza hukumu.Slobodan Praljak, 72, alikuwa mmoja wa viongozi sita wa zamani wa kisiasa na wa kijeshi wa Bosnia wa asili ya Croatia ambao walikuwa wamefika mahakamani.Amefariki akitibiwa hospitalini na Umoja wa Mataifa umesema sasa mahakama hiyo ni "eneo la uhalifu".Alikuwa amehukumiwa kufungwa jela miaka 20 mnamo 2013 kwa makosa ya uhalifu wa kivita yaliyotekelezwa katika mji wa Mostar.Baada ya kusikiliza hukumu kwamba majaji walikuwa wamedumisha kifungo hicho, alimwambia jaji, "Nimekunywa sumu".Sita hao walikuwa wanasikiliza uamuzi wa mwisho wa rufaa uliokuwa unatolewa na mahakama maalum ya kimataifa ya UN iliyokuwa inashughulikiwa makosa yaliyotekelezwa Yugoslavia (ICTY).Ingawa walikuwa washirika dhidi ya Waserbia wa Bosnia wakati wa vita hivyo vya 1992-95, Wacroatia wa Bosnia na Waislamu walipigana wenyewe kwa wenyewe kwa miezi 11.Praljak alisimama na akainua mkono wake hadi kwenye kinywa chake, kisha anainamisha kichwa chake nyuma na kuonekana kunywa kitu kutoka kwenye gilasi ndogo.Jaji mwandamizi Carmel Agius mara moja alisitisha shughuli na gari la kuwabeba wagonjwa likaitwa."Sawa," jaji alisema. "Tunaahirisha ki...Tunaahirisha...Tafadhari, pazia. Usiondoe gilasi ambayo ameitumia alipokunywa kitu."Kabla ya pazia kurejeshwa, ukumbi wa mahakama umeonekana kujawa na mkanganyiko, anasema mwandishi wa BBC Anna Holligan kutoka The Hague.Gari la kuwabeba wagonjwa lilionekana baadaye likifika nje ya ukumbi wa mahakama huku helikopta ikipaa juu angani.Wafanyakazi kadha wa uokoaji wameingia ukumbini na vifaa vyao.Uhalifu dhidi ya WaislamuPraljak, kamanda wa zamani wa wahudumu wakuu wa Jeshi la Walinzi wa Wacroatia wa Bosnia (HVO), alifungwa kwa makosa ya jinai dhidi ya binadamu.Baada ya kufahamishwa kwamba wanajeshi walikuwa wanawakamata Waislamu Prozor majira ya joto 1993, alikosa kuchukua hatua zozote za maana kuzuia hilo, mahakama hiyo ya UN ilisema.Aidha alikosa kuchukua hatua hata baada ya kupashwa habari kwamba mauaji yalikuwa yamepangwa, pamoja na mashambulio dhidi ya wafanyakazi wa mashirika ya kimataifa na kuharibiwa kwa daraja la kale la mji wa Mostar na misikiti.Mahakama ya ICTY ambayo iliundwa 1993 itamaliza kati yake mwisho wa mwaka huu. Kikao cha kusikiliza rufaa iliyowasilishwa na washtakiwa wa uhalifu wa kivita mjini The Hague, Uholanzi kimesitishwa ghafla baada ya mmoja w... Soma zaidi » Kimataifa
Tweet Share Share Share Share Share Kikwete kutohudhuria kuapishwa kwa Kenyatta. Unknown November 28, 2017 Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete amesikitika kutohudhuria kuapishwa kwa Rais mteule wa Kenya na kusema alipata mwaliko kuhudhuria sherehe za kuapishwa Kenyatta lakini ameshindwa kutokana na kuingiliana kwa majukumu.Leo baadhi ya mitandao ya kijamii nchini Kenya alidai kuwa Rais mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete ni mmoja wa wageni ambao wamehudhuria sherehe za kuapishwa kwa Uhuru Kenyatta jambo ambalo Jakaya Kikwete amelipinga kwa kusema ameshindwa kwenda Kenya kutokana na majukumu kuingiliana.Jakaya Kikwete ametumia mtandao wake wa Twitter kufikisha ujumbe wake wa pongezi kwa Kenyatta kuchaguliwa tena kuongoza nchi ya Kenya ambayo ni nchi rafiki na Tanzania kwa miaka mingi sasa."Nakupongeza Rais UKenyatta kwa kuchaguliwa tena kuongoza nchi rafiki ya Kenya. Nakushukuru kwa mwaliko wa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwako. Nasikitika sitaweza kuhudhuria kutokana na kuingiliana kwa majukumu. Nakutakia kila la kheri katika awamu yako ijayo" alindika KikweteRais Uhuru Kenyatta alichaguliwa kuwa Rais kwa Kenya katika uchaguzi wa marudio uliofanyika Oktoba 26, 2017 Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete amesikitika kutohudhuria kuapishwa kwa Rais mteule wa Kenya na kusema alipata mwaliko kuhud... Soma zaidi » Kimataifa
Tweet Share Share Share Share Share Makamu wa Rais ahudhuria kuapishwa kwa Rais Kenyatta. Unknown November 28, 2017 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo asubuhi tarehe 28 Novemba, 2017 amewasili Mjini Nairobi nchini Kenya ambako anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba amepokelewa na Mhe. Balozi Robinson Njeru Githae wa Kenya na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. Pindi Chana.Sherehe za kuapishwa kwa Mhe. Rais Uhuru Kenyatta zinafanyika katika uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi.Gerson MsigwaMkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULUNairobi28 Novemba, 2017 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo asubuhi tarehe 28 Novemba, 2017 amewasili Mjini Nairobi nchin... Soma zaidi » Kimataifa
Tweet Share Share Share Share Share Papa Francis aizuru Myanmar. Unknown November 27, 2017 Papa Francis anaanza ziara ya wiki nzima nchini Myanmar na Bangladesh leo Jumatatu, wakati wasiwasi unaendelea wa kimataifa kuhusu usalama na ulinzi kwa wasilamu wa Rohingya.Anatarajiwa kukutana na Aung Sun Suu Kyi na mkuu wa jeshi Myanmar.Hata kabla ya kuondoka Roma, Papa Francis alikuwa anakabailiwana kitendawili cha kidiplomasia: iwapo kuliita kundi dogo la waislamu Myanmar - Rohingya.Ni jina lisilo tumika na serikali ya kiraia na jeshi - wakieleza kuwa ni wahamiaji haramu kutoka Bangladesh na kwahivyo hawapaswi kuorodheshwa kama mojawapo ya makabila nchinihumo.Lakini mashirika ya kutetea haki za binaadamu wanamuomba awaite hivyo, yakieleza kuwa nilazima Papa Francis aoneshe huruma kwa watu walionyimwa uraia na tangu Agosti wamekabiliwa na kile kamishna wa haki za binaadamu katika Umoja wa mataifa amekitaja kuwa 'kinachoonekana kuwa mauaji ya kikabila'.Amnesty:Burma yatega mabomu kuwazuia RohingyaMapungufu ya UN katika mzozo wa RohingyaWapiganaji wa Rohingya watangaza kusitisha mapigano, MyanmarMyanmar yatakiwa kukoma kuwatesa Waislamu wa RohingyaZaidi ya WaRohingya 600,000 wamekimbilia mpakani - na wakimbizi wakielezea kukabiliwa na mauaji, ubakaji na kuteketezwa moto kwa vijiji - jeshi imekana tuhuma zote.Papa atakutana na kiongozi wa Myanmarr - Aung Sun Suu Kyi - Jumanne - huenda ni jukumu zito kidiplomasia katika miaka yake minne kama kiongozi wa kanisa katoliki. Papa Francis anaanza ziara ya wiki nzima nchini Myanmar na Bangladesh leo Jumatatu, wakati wasiwasi unaendelea wa kimataifa kuhusu usalama n... Soma zaidi » Kimataifa
Tweet Share Share Share Share Share Hofu yatanda, kwa mlima wa volkano kulipuka Bali. Unknown November 27, 2017 Takriban watu laki moja karibu na mlima Agung kisiwani Bali wametakiwa kuhama wakati maafisa wanahofia mlima huo wa volkano kulipuka pakubwa.Maafisa Indonesia wameongeza kiwango cha hatari na kupanua zaidi eneo linalokaribiana na mlima huo wa vokano unoendelea kuchemka linalotarajiwa kuathirika.Uwanja wa ndege wa kipekee katika kisiwa hicho maarufu cha utalii cha Bali umefungwa.Majivu na moshi wa Volcano hiyo imefikia urefu wa zaidi ya mita 3400 juu ya mlima huo hali iliyosababisha giza.Hatari kwa ndege baada ya Volkano BaliHofu ya kulipuka volkano katika kisiwa cha kitalii cha BaliMlima huo uitwao Agung ulirusha majivu mengi na kutandaza mvuke na moshi mwingi mara ya pili katika kipindi cha wiki moja.Maafisa wamehimiza na kuwasaidia maelfu ya wakaazi na watalii kulihama eneo hilo na kwenda kwingine.Mlima huo wa volkano ulionekana ukitoa moshi na sauti za milipuko zilisikika kwa umbali wa kilomita 12 kutoka juu ya mlima huo."Miale ya moto inazidi kutizamwa usiku kucha. Hii inaashiria uwezekano wa mlipuko mkubwa zaidi ," imesema taarifa ya bodi ya kitafa ya usimamizi wa majanga Indonesia, katika ukurasa wake wa Facebook.Mwaka 1963 mlima huo ulilipuka na kusababisha vifo vya takriban watu 1,600. Takriban watu laki moja karibu na mlima Agung kisiwani Bali wametakiwa kuhama wakati maafisa wanahofia mlima huo wa volkano kulipuka pakubwa... Soma zaidi » Kimataifa
Tweet Share Share Share Share Share Ziwa Victoria hatarini kukauka. Unknown November 27, 2017 Hii ni baada ya wanasayansi kusema kwamba ziwa kubwa zaidi barani Afrika ziwa Victoria linalounganisha nchi za Tanzania, Kenya na Uganda, lipo katika hatari kubwa ya kukauka kwa maji yake.Wanasema kwamba sababu kubwa. itakayopelekea ziwa kukauka ni uvuvi haramu na uliopitiliza pamoja na uvamizi wa mazingira kuzunguka maeneo ya ziwa.Maji machafu pia yanayotiririshwa kuelekea kwenye ziwa yanahatarisha usalama wa viumbe wanaopatikana katika ziwa hilo.Kwa upande wa pili jeshi la Uganda limeweka mipango maalum ikiwa ni pamoja na kuharibu nyenzo za uvuvi zinazotajwa kuwa miongoni mwa sababu. Hii ni baada ya wanasayansi kusema kwamba ziwa kubwa zaidi barani Afrika ziwa Victoria linalounganisha nchi za Tanzania, Kenya na Uganda, li... Soma zaidi » Kimataifa
Tweet Share Share Share Share Share Rais Trump ajibiwa na CNN, kuhusu tweet yake. Unknown November 26, 2017 Rais wa Marekani Donald Trump amekishutumu kituo cha habari cha CNN kwa kusambaza habari za uongo kuhusu Marekani ulimwenguni.Rais Trump katika mtandao wake wa twitter amechapisha chapisho lake kwa kuandika kuwa CNN ni "Fake News".Trump ametoa sifa kwa kituo cha habari cha Fox News na kusema kuwa ni kituo kinachoheshimika zaidi Marekani.Trump ameongezea kwa kusema japokuwa CNN haina heshima kubwa Marekani, inatizamwa na ulimwengu mzima na hivyo kupotosha nchi nyingine kuhusu nchi yake ya Marekani.Hata hivyo kitengo cha mawasiliano cha CNN kimejibu chapisho aliloliandika trump katika ukurasa wake wa twitter na kuandika,"Sio kazi yetu kuiwakilisha Marekani ulimwenguni,ni kazi yako wewe.Sisi tunafikisha habari tu".Kwa muda sasa Trump amekuwa akishambuliwa na kituo hicho cha habari. Rais wa Marekani Donald Trump amekishutumu kituo cha habari cha CNN kwa kusambaza habari za uongo kuhusu Marekani ulimwenguni. Rais Trump ka... Soma zaidi » Kimataifa
Tweet Share Share Share Share Share Zimbabwe: Morgan Tsvangirai aomba Mugabe kusamehewa Unknown November 25, 2017 Kiongozi wa chama cha ZANU-PF Lovemore Matuke amesema kuwa hakushiriki katika harakati za kumuondoa Mugabe madarakani.Kwa mujibu wa habari,Matuke amesema kuwa Mugabe na familia wako salama na daima atakumbukwa kama shujaa.Wakati huohuo kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai amewataka wananchi wamsamehe Mugabe.Morgan Tsvangirai amesema kuwa ni vyema Mugabe akasamehewa na taifa kwani si taifa halijengwi kwa kulipiza visasi. Kiongozi wa chama cha ZANU-PF Lovemore Matuke amesema kuwa hakushiriki katika harakati za kumuondoa Mugabe madarakani. Kwa mujibu wa habari,... Soma zaidi » Kimataifa
Tweet Share Share Share Share Share Shambulio la Msikiti laua 235 Misri Unknown November 24, 2017 Wanamgambo wametekeleza shambulio la bomu na ufyatuaji wa risasi katika msikiti mmoja uliopo kaskazini mwa eneo la Sinai na kuwaua takriban watu 235 kulingana na chombo cha habari cha taifa.Walioshuhudia wanasema kuwa msikiti wa al-Rawda katika mji wa Bir al-Abeid , karibu na al-Arish ulilengwa wakati wa ibada ya Ijumaa.Maafisa wa polisi wanasema kuwa wanaume wanne waliokuwa ndani ya gari moja waliwafyatulia risasi waliokuwa wakiabudu kulingana na chombo cha habari cha AP.Misri imekuwa ikikabiliana na wanamgambo katika eneo hilo tangu 2013.Kumekuwa na mshambulio ya mara kwa mara yanayolaumiwa kutekelezwa na wanamgambo katika rasi ya Sinai lakini hilo ni shambulio baya zaidi kuwahi kufanyika.Ripoti moja inasema kuwa waliolengwa ni wafuasi wa maafisa wa usalama waliokuwa wakitekeleza ibada katika msikiti huo.Wakazi wa eneo hilo wanasema kuwa wafuasi wa madhehebu ya Sufi hukongamana katika msikiti huo.Makundi ya wanajihad likiwemo lile la Islamic State wanawaona wasufi kama watu wasioamini.Rais Abdul Fattah al-Sisi anatarajiwa kukutana na maafisa wa usalama kuzungumzia kisa hicho . Wanamgambo wametekeleza shambulio la bomu na ufyatuaji wa risasi katika msikiti mmoja uliopo kaskazini mwa eneo la Sinai na kuwaua takriban ... Soma zaidi » Kimataifa