Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis jana ametoa mwito wa kuwepo amani katika mji wa Jerusalem wakati wa salamu zake za Krismasi.

Na kuelezea hali watoto wanayokabiliwa nayo katika maeneo yenye migogoro huku pia akitoa mwito kwa waumini bilioni 1.3 wa kanisa katoliki duniani kote kutowapuuza wahamiaji.

Akiwahutubia mamia kwa maelfu ya waumini wa kanisa hilo mjini Vatican Papa Francis ametoa mwito wa amani mjini Jerusalem na katika ardhi yote takatifu.

Amesema ulimwengu unashuhudia watoto katika Mashariki ya Kati wakiendelea kuteseka kwasababu ya mivutano kuongezeka kati ya waisrael na wapalestina.

Papa Francis amesema ulimwengu unapaswa kuomba ili majadiliano ya pande zinazovutana yarejee na hatimaye suluhisho la mataifa mawili lipatikane na ambalo litatambuliwa kimataifa.


Ujumbe huo wa papa katika mkesha wa krismasi umekuja mnamo wakati mivutano mipya ikiibuka katika ukingo wa magharibi kufuatia rais Donald Trump kutangaza kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel huku pia rais wa Guatemala Jimmy Morales akisema nchi yake itahamishia ubalozi wake mjini humo.

Post a Comment

Powered by Blogger.