Bodi
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inawataarifu wanafunzi
wanaonufaika na mikopo kuwa wanatakiwa
kuendelea kuingiza taarifa zao kwa njia ya mtandao kupitia
http://olas.heslb.go.tz hadi tarehe 31
Januari, 2018.
Wanafunzi wanufaika wanapaswa kufanya yafuatayo:
• Tembelea
mtandao wa http://olas.heslb.go.tz
• Fungua
kiunganishi cha “Click here to start” kwenye maelezo ya mwanzo ya kukaribisha.
• Weka
namba yako ya mtihani ya Kidato cha Nne na mwaka uliofanya mtihani huo, kwa
mfano: S0129.0004.2020
• Weka namba
yako ya akaunti ya Benki kama ilivyowasilishwa HESLB au kama inavyoonekana
kwenye “signing sheet”
• Ingiza
neno jipya la siri na ulithibitishe.
• Baada ya
kuthibitisha, ukurasa wa kuweka picha yako “passport size photo” utafunguka.
• Weka
picha yako ya rangi katika ukubwa wa 120×150
• Wanufaika
wapya wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/2018 hawatahusika kwenye zoezi hili
kwa vile taarifa zao ziliwasilishwa wakati wa kuomba mikopo.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Tarehe 26/01/2018
Post a Comment