Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Freeman Mbowe amewataka wagombea wote wa udiwani katika kata tano Arumeru Mashariki wajitoe katika uchaguzi mdogo wa madiwani.
Mbowe ametoa rai hiyo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mkoani Arusha kwa kudai kuwa uchaguzi huo umegubikwa na vurugu.
Sambamba na hayo Freeman Mbowe amewataka mawakala wao wa uchaguzi walioko katika vituo vya kupigia kura waondoke vituoni.
Leo wananchi wa Tanzania Bara wanapiga kura kuchagua madiwani katika kata 43 hapa nchini, hadi wakati huu pamekuwa na taarifa mbalimbali za uvunjifu wa amani na ukiukwaji wa haki, ikiwemo kukamatwa kwa baadhi ya wagombea na mawakala wao.
Post a Comment