Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), kimedai kuwa Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob amekamatwa na polisi wakati uchaguzi mdogo wa madiwani ukiendelea katika Kata ya Saranga.
Baada ya kukamwatwa kwa Boniface Jacob, msemaji wa chama hicho, Tumaini Makene amesema haijulikani meya huyo amepelekwa katika kituo gani na hawafahamu ni sababu ipi iliyopelekea meya huyo kushikiliwa na polisi.
Amesema Jacob aliapishwa kuwa wakala wa mgombea wao wa kiti cha udiwani katika majumuisho ya uchaguzi wa Kata ya Saranga hivyo alikuwa anahusika katika uchaguzi unaoendelea katika kata hiyo.
Makene amesema uongozi wa chama chao unafuatilia ili kufahamu sababu za kukamatwa kwake na ni wapi alipo meya Manispaa ya Ubongo.
"Sasa kama mtu tunayemtegemea kuwa wakala kwenye majumuisho ya kuhesabu kura unategemea nini, hizi ni rafu ambazo mamlaka husika zinatakiwa kufuatilia", amesema Makene.
Post a Comment