Rais wa Marekani Donald Trump amekishutumu kituo cha habari cha CNN kwa kusambaza habari za uongo kuhusu Marekani ulimwenguni.
Rais Trump katika mtandao wake wa twitter amechapisha chapisho lake kwa kuandika kuwa CNN ni "Fake News".
Trump ametoa sifa kwa kituo cha habari cha Fox News na kusema kuwa ni kituo kinachoheshimika zaidi Marekani.
Trump ameongezea kwa kusema japokuwa CNN haina heshima kubwa Marekani, inatizamwa na ulimwengu mzima na hivyo kupotosha nchi nyingine kuhusu nchi yake ya Marekani.
Hata hivyo kitengo cha mawasiliano cha CNN kimejibu chapisho aliloliandika trump katika ukurasa wake wa twitter na kuandika,"Sio kazi yetu kuiwakilisha Marekani ulimwenguni,ni kazi yako wewe.Sisi tunafikisha habari tu".

Post a Comment