Tweet Share Share Share Share Share Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Kilimba Amepata Ajali na Familia Yake Unknown December 25, 2017 M/kiti CCM Mkoa wa Singida, ndugu Juma Kilimba amepata ajali akitumia gari lake binafsi akiwa na familia yake, Mke wake na watoto wawili wamepewa rufaa.Yeye bado na watoto wawili bado wako hospital ya Wilaya Kiomboi ambapo mtoto mmoja hawezi kusafirishwa hali yake sio nzuri. M/kiti CCM Mkoa wa Singida, ndugu Juma Kilimba amepata ajali akitumia gari lake binafsi akiwa na familia yake, Mke wake na watoto wawili wam... Soma zaidi » Singida
Tweet Share Share Share Share Share Wajasilamali kutoka mkoa wa singida wakikabithiwa vyeti kwenye semina Unknown November 25, 2017 Baadhi ya mujasiliamali akipokea cheti kutoka kwa mgeni rasmi katika ukumbi wa RC katoliki singida mjini, hiyo semina imezungumzia mambo mengi ikiwemo kutengeneza batiki, karanga, sabuni ya majivu, sabuni ya maji. washiriki walikuwa ni wengi sana ambao wamejitokeza kushiriki katika semina hiyo ya ujasiliamali . Baadhi ya mujasiliamali akipokea cheti kutoka kwa mgeni rasmi katika ukumbi wa RC katoliki singida mjini, hiyo semina imezungumzia mambo men... Soma zaidi » Singida
Tweet Share Share Share Share Share Bwana harusi afariki, mkewe ajeruhiwa katika ajali wakitoka kufunga ndoa Unknown November 25, 2017 Watu 12 wamekufa na wengine 22 kujeruhiwa katika ajali iliyotokea kijiji cha Ighuka wilayani Ikungi kwenye Barabara Kuu ya Singida – Manyoni baada ya Toyota Hiace waliyokuwa wakisafiria kutoka kumchukua bibi harusi kugongana uso kwa uso na Toyota Noah iliyokuwa imepakia watu kutoka msibani.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Debora Magiligimba alisema kuwa ajali hiyo ilitokea juzi saa mbili usiku kwa kulihusisha gari lenye namba za usajili T 581 BBV iliyokuwa ikitokea Singida kwenda Manyoni na T 423 CFF iliyokuwa ikitokea Manyoni kwenda Singida.Alisema kuwa ingawa uchunguzi wa kina juu ya chanzo cha ajali hiyo bado unaendelea, taarifa za awali zinaonesha kuwa sababu kuu ni mwendo kasi na uzembe wa madereva.“Baadhi ya majeruhi walituambia dereva wa Toyota Hiace aliyekuwa anatoka Singida mjini alihama kutoka upande wake na kwenda upande wa pili wa barabara ambako aligongana uso kwa uso na Noah iliyokuwa imebeba watu waliokuwa wakitoka msibani na kusababisha vifo vya abiria 10 hapo hapo na majeruhi 24,” alisema.Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa mkoa wa Singida, Dk Ng’hungu Kusenza alisema kuwa majeruhi wawili waliofikishwa Hospitali ya Misheni Puma kwa ajili ya matibabu pia walikufa hivyo kufanya idadi ya watu waliokufa kuwa 12.Aliwataja waliokufa ambao miili yao imehifadhiwa Hospitali ya mkoa kuwa ni John Duma, Jasson Nsunza, Abubakar Omari, Mary Kinku, Mwanaidi Juma na Husna Juma, Wengine ambao miili yao imehifadhiwa Hospitali ya Misheni Puma wilayani Ikungi ni Ezekiel Joseph, Mussa Daniel, Namtaki Daniel, Hamis Omari, Jumanne Mganga na Wansola Shalua. Habari ambazo hazijathibitishwa zinadai kuwa Bwanaharusi na madereva wa magari yote mawili ni miongoni mwa watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo.Chanzo: Habarileo Watu 12 wamekufa na wengine 22 kujeruhiwa katika ajali iliyotokea kijiji cha Ighuka wilayani Ikungi kwenye Barabara Kuu ya Singida – Manyoni... Soma zaidi » Singida