Tweet Share Share Share Share Share Wenger amtetea Alexis Sanchez baada yake kukosa kupimwa. Unknown January 26, 2018 Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amemtetea mchezaji wa zamani wa klabu hiyo aliyehamia Manchester United baada yake kukosa kipimo muhimu kuhusu matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwilini. Aidha, amesema klabu hiyo haifichi habari zozote kuhusu tukio hilo. Raia huyo wa Chile mwenye miaka 29 anadaiwa kukosa kipimo muhimu Jumatatu siku ambapo alikamilisha uhamisho wake kwenda Manchester United. "Nafikiri lilikuwa tukio la kipekee, kwake kukosa kipimo siku hiyo kwa sababu alikuwa kwingine," amesema Wenger. Mfaransa huyo ameongeza pia kwamba klabu yake haijaombwa ufafanuzi wowote na Chama cha Soka cha England au Shirika la kupambana na matumizi ya dawa zilizoharamishwa michezoni Uingereza. Sanchez alihamia Gunners kutoka Barcelona mwaka 2014, lakini alielekea Old Trafford kwa kubadilishana na mchezaji wa Armenia Henrikh Mkhitaryan. Baada ya taarifa za awali Uhispania, magazeti ya Uingereza Alhamisi yaliripoti kwamba Sanchez alikiuka kanuni FA ya kupatikana wakati wowote ule anapotakiwa kupimwa. Sanchez na Mkhitaryan walipigwa picha wakiwa afisi za uhamiaji Liverpool wakitafuta vibali vya kufanya kazi kabla ya kukamilisha uhamisho wake. Wenger amesema: "Jumatatu kulikuwa na mengi sana yaliyokuwa yanatokea, ni siku ya kipekee sana kwa Alexis Sanchez - kujaza stakabadhi muhimu, vibali vya kazi na usafiri. Alikuwa bado ni mchezaji wetu Jumatatu au la? Huwezi kujua. "Ni siku mbaya tu kwako kutafutwa ukapimwe. Kusema kweli, ukiangalia upande wa usimamizi, huenda ikawa bado ilikuwa ni wajibu wetu kwa kuwa hakuwa amehama. Sijui nini hasa kilitokea. "Sina wasiwasi kwa sababu hatuna chochote cha kuficha, huwa tunajaribu sana kadiri ya uwezo wetu kushirikiana na maafisa wa kupambana na matumizi ya dawa zilizoharamishwa michezoni Uingereza. "Nia ya Alexis haikuwa kujificha na sisi hatuna jambo la kuficha." Sheria zinasemaje? Klabu zinatakiwa kutoa maelezo sahihi ya kina kuhusu vipindi vya mazoezi na walipo wachezaji ili waweze kupimwa wakati wowote ule. Klabu ikikosa kufanya hivyo - au maafisa wa kupima wachezaji washindwe kumpata mchezaji wanayemtafuta - mara tatu kipindi cha miezi 12, basi huchukuliwa kwamba amekiuka sheria za FA. Manchester City na Bournemouth mwaka jana walitozwa faini ya £35,000 kila mmoja na kutahadharishwa baada ya kukiuka kanuni hizo. Arsenal wamemnunua yeyote? Wenger amesema hawapo karibu kumnunua mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang. Ofa yao ya pili ya euro 50m (£43.64m) ilikataliwa wiki hii. Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amemtetea mchezaji wa zamani wa klabu hiyo aliyehamia Manchester United baada yake kukosa kipimo muh... Soma zaidi » Michezo
Tweet Share Share Share Share Share Kenyatta ateua mawaziri wapya Kenya, na balozi mpya Tanzania. Unknown January 26, 2018 Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza watu anaopendekeza waidhinishwe kuwa mawaziri katika serikali yake mpya baada yake kushinda uchaguzi mwaka jana. Mawaziri sita ambao walikuwa wanahudumu katika serikali yake muhula uliopita wamevuliwa uwaziri na kuteuliwa kuwa mabalozi. Bw Dan Kazungu, ambaye amekuwa waziri wa madini, amependekezwa kuwa balozi mpya wa Kenya nchini Tanzania. Aliyekuwa balozi wa Kenya nchini humo Chirau Ali Mwakwere alijiuzulu mwaka jana ili kuwania kiti cha ugavana katika uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti. Alishindwa kwenye uchaguzi huo. Miongoni mwa walioteuliwa kuwa mawaziri wapya ni mwanahabari mkongwe Farida Karoney ambaye ameteuliwa kuwa waziri wa ardhi. Wadhifa huo ulikuwa unashikiliwa na Prof Jacob Kaimenyi ambaye amependekezwa kuwa balozi wa Kenya katika Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Sayansi, Elimu na Utamaduni (Unesco) mjini Geneva. Bi Monica Juma ameteuliwa kuwa waziri mpya wa mambo ya nje kuchukua nafasi ya Amina Mohamed ambaye amependekezwa kuwa waziri wa elimu. Mawaziri walioteuliwa kuwa mabalozi Judi Wakhungu (Mazingira) - Ufaransa Cleopa Mailu (Afya) - Umoja wa Mataifa mjini Geneva Dan Kazungu (Madini) - Tanzania Phylis Kandie (Leba na Jumuiya ya Afrika Mashariki) - Ubelgiji, Luxemburg na Umoja wa Ulaya Willy Bett (Kilimo) - India Jacob Kaimenyi (Ardhi) -UNESCO, Paris Hassan Wario (Michezo) - Austria Kwa sasa, orodha kamili ya mawaziri waliopendekezwa ni: Adan Mohammed - Viwanda Amina Mohammed - Elimu Charles Keter - Kawi Eugene Wamalwa - Ugatuzi Farida Karoney - Ardhi Fred Matiangi - Masuala ya Ndani na Usalama Henry Rotich - Fedha (Hazina Kuu) James Macharia - Uchukuzi John Munyes - Madini na Mafuta Joseph Mucheru - Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Keriako Tobiko - Mazingira Margaret Kobia - Vijana na Utumishi wa Umma Monica Juma -Mambo ya Nje Mwangi Kiunjuri - Kilimo Najib Balala - Utalii Peter Munya - Jumuiya ya Afrika Mashariki Racheal Omamo - Ulinzi Raphel Tuju - Waziri (Bila wizara kwa sasa) Rashid Achesa - Michezo Sicily Kariuki - Afya Simon Chergui - Maji Ukur Yattany - Leba Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza watu anaopendekeza waidhinishwe kuwa mawaziri katika serikali yake mpya baada yake kushinda ... Soma zaidi » Kimataifa
Tweet Share Share Share Share Share Jibu la Polisi baada ya kuagizwa na Waziri kuwakamata watuhumiwa ndani ya siku 7. Unknown January 26, 2018 Jeshi la Polisi limesema limepokea agizo la Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla la kuwachukulia hatua watu wanne ndani ya siku saba kwa madai wanashiriki katika mtandao wa ujangili, lakini halifanyi kazi kwa shinikizo. Msemaji wa Jeshi hilo, Barnabas Mwakalukwa amesema polisi wanafanya kazi kwa kufuata kanuni, taratibu na sheria za Jeshi hilo. Juzi, Kigwangalla mbali na kutoa agizo hilo, amesema watu hao wanne pia walipanga njama za kumuua mwanaharakati, Wayne Lotter na kwamba polisi wakishindwa kuwakamata atawashtaki kwa Amiri Jeshi Mkuu ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mwakalukwa amesema jukumu lao ni kukamata wanapopata shitaka la kuwapo kwa kitu kisicho cha kawaida, kuchunguza na kupeleka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya kukamilisha taratibu nyingine. “Kazi yetu ni kukamata, kuchunguza na kupeleka kwa DPP kwa ajili ya taratibu nyingine, hatufanyi kazi kwa matamko ya bungeni,” amesema na kuongeza; “Alichokisema mheshimiwa Kigwangalla nimekisoma kwenye vyombo vya habari akihusisha na suala la mwanaharakati aliyeuawa, sisi hatufanyi kazi kwa kufuata vyombo vya habari vimeandika nini au limetolewa tamko gani au kuna shinikizo gani, tunafanya kwa kufuata taratibu zilizopo.” Jeshi la Polisi limesema limepokea agizo la Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla la kuwachukulia hatua watu wanne nd... Soma zaidi » Kitaifa
Tweet Share Share Share Share Share Taarifa muhimu kwa wanafunzi wa vyuo kutoka Bodi ya Mikopo (HESLB). Unknown January 26, 2018 Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inawataarifu wanafunzi wanaonufaika na mikopo kuwa wanatakiwa kuendelea kuingiza taarifa zao kwa njia ya mtandao kupitia http://olas.heslb.go.tz hadi tarehe 31 Januari, 2018. Wanafunzi wanufaika wanapaswa kufanya yafuatayo: • Tembelea mtandao wa http://olas.heslb.go.tz • Fungua kiunganishi cha “Click here to start” kwenye maelezo ya mwanzo ya kukaribisha. • Weka namba yako ya mtihani ya Kidato cha Nne na mwaka uliofanya mtihani huo, kwa mfano: S0129.0004.2020 • Weka namba yako ya akaunti ya Benki kama ilivyowasilishwa HESLB au kama inavyoonekana kwenye “signing sheet” • Ingiza neno jipya la siri na ulithibitishe. • Baada ya kuthibitisha, ukurasa wa kuweka picha yako “passport size photo” utafunguka. • Weka picha yako ya rangi katika ukubwa wa 120×150 • Wanufaika wapya wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/2018 hawatahusika kwenye zoezi hili kwa vile taarifa zao ziliwasilishwa wakati wa kuomba mikopo. Imetolewa na: Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU Tarehe 26/01/2018 Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inawataarifu wanafunzi wanaonufaika na mikopo kuwa wanatakiwa kuendelea kuingiz... Soma zaidi » Kitaifa
Tweet Share Share Share Share Share Tazama Vichwa Vya Habari Katika Magazeti ya leo Jumamosi, January 27, 2018. Unknown January 26, 2018 Habariniza Asubuhi, ni Siku nyingine tena na Karibunikatika Magazeti ya Leo Tanzania Jumamosi, January 27 2018 kuanzia ya Dini, Udaku, Michezo na Hardnews kujionea yote Makubwa yaliyojiri. Habarini za Asubuhi , ni Siku nyingine tena na Karibuni katika Magazeti ya Leo Tanzania Jumamosi , January 27 2018 kuanzia ya Dini... Soma zaidi » Magazeti